Kwa kusaini hii fomu ya kujiunga na RAMADAN FUN RUN (“Tukio”), mshiriki anakubali na kuridhia yafuatayo:-
1. Pamoja nakwamba waandaaji wamechukua tahadhari zote kuhakikisha usalama wa Washiriki ajali na hatari zinaweza kutokea, hivyo washiriki kwa
ridhaa yao wenyewe wanaafiki kushiriki katika matembezi haya wakitambua uwezekano wa hatari na ajali kutokea na kwa ajili hiyo wanatoa kinga ya
kutodai fidia au madai ya aina yoyote kutokana naTukio hili au kwa namna yoyote, pamoja na pasipo ukomo kwa Waandaaji, Wafadhili, Watangazaji,
Serikali za Mitaa, au Mamlaka yoyote pamoja na Wakurugenzi, Wafanyakazi, Wagavi na wasaidizi wao wote waliotajwa hapa, pamoja na mtu binafsi, Afisa
au Wakala (“Wahusika”).
2. Mshiriki wa Tukio anatoa kinga na anaahidi kutodai fidia wala madai ya aina yoyote yale iwe yamesababishwa mojakwamoja au la, iwe imesababishwa
kwa uzembe au la, au kwakushiriki au kuhusika katika kupita njia au kwaTukio au kwa namna nyingine ikijumuisha ucheleweshaji, usumbufu, ajali, kifo,
kuumia, ugonjwa kwa watu wao, au hasara au uharibifu kwenye mali au gharama na matumizi yaliyofanyika, kufanyika au kuwekwa na Washiriki na/au
mtoto yeyote yule chini ya uangalizi au usimamizi wa Washiriki.
3. Mshiriki anathibitisha kuwa na uwezo kiafya na kiakili na ana Mamlaka ya kusaini hii fomu ya usajili na kukubaliana na masharti haya.
4. Mshiriki ninatoa ruhusa na ridhaa ya kutumia pasipo malipo au madai ya aina yoyote, jina langu, sauti, picha yangu inayosimama na inayotembea, itumikwe katika matangazo, mawasiliano ya aina yoyote ile, promosheni, au aina nyingine yoyote ile ya matangazo ya sasa na kwa matukio ya baadaye.
5. Mzazi/Msimamizi wanao waruhusu watoto kushiriki ni lazima wasaini fomu hii na itamaanisha kukubalina kuafiki kuwa mtoto atashiriki kwa masharti
na vigezo vya Tukio hili, na aidha kutofidia kwa Wahusika kwa kiwango, iwapo kipo, ambacho mtoto hataweza kuondoa haki na madai yake kama
yalivyoelezwa humu.