The Garden Grant ni ruzuku ya Sanaa inayokualika utengeneze kitu kizuri. Tunakaribisha ufahamu mpana kuhusu dhana ya Sanaa. Tunafadhili miradi ya muda mfupi na tunapendekeza miradi anuwai ya ubunifu wa taaluma nyingi. The Garden Grant inatuzwa wabunifu huru na imelengwa kuwanufaisha watu binafsi wenye mawazo ya kupendeza na kwa hivyo si sharti mtu awe na chombo cha 501 (c)(3) au uhusiano na yeyote yule ili kutuma ombi.
Wakati kama huu tunatoa kipaumbele kwa waombaji anuwai; kwa hivyo wabunifu wenye mwelekeo wa usenge au wanaotoka jamii zilizowekwa pembeni kwa ajili ya rangi wanahimizwa kuomba ruzuku. Mkuu wa kimataifa wa ruzuku ya The Garden Grant anaungwa mkono na shirika la Ford Foundation na kwa hivyo tunafurahia kupokea maombi kutoka nchi za Kenya, Ghana na Mexico.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara:
1. Ni nani mwanzilishi?
The Garden Grant ni mpango wa vyombo vya habari vya Maacah. Tazama tovuti:
www.maacah.com**Zingatia: Wafadhili wanachaguliwa na jopo la watu watano wenye taaluma za ubunifu.
2. Nini kinachohitajika?
Ikiwa ufadhili utafanikiwa, tunataka kuona tu kile ambacho umetengeneza. Hii ina maana kwamba unafaa kumaliza mradi uliopendekeza. Hatudai umiliki wa mradi wako nahutakiwi kuulipia. Si mkopo wala uwekezaji. Tunachotaka tu ni kwamba ukubali ruzuku The Garden Grant na washirika wake (vyombo vya habari vya Maacah) kusambaza kazi yako na wajisifu juu yako.
3. Ni miradi ipi ambayo ruzuku ya The Garden Grant inatafuta kuunga mkono?
Kuonyesha furaha: tunaamini kuwa kitu kisicho cha kawaida ni muhimu; hata hivyo una uhuru wa kufafanua kwa ubunifu maana ya Sanaa ikiwa kwa maandishi, video, Upishi, mchongo, au chochote kile. Unaweza kuomba hadi Shilingi 10,000 – 1,098,500 za Kenya, Ḉ 60,164 za Ghana na Ṩ 200,680 za Mexico.
Hata hivyo Bodi ya Ukaguzi itaamua kiwango utakachopewa. Lengo maalumu ni kukamilisha mradi kwa wakati lakini kwa jumla miradi yote inafaa kumalizwa kwa muda wa mwaka mmoja wa ufadhili.
4. Je, naweza kutumia ufadhili huu kupanua miradi mingine niliyo nayo?
Ndio, unaweza kuonyesha kile ulichokuwa ukifanyia kazi na jinsi ruzuku itakavyokusaidia kumaliza au kupanua mawazo yako.
5. Ikiwa una maswali ambayo hatujayajibu basituletee kupitia anwani ifuatayo:
hello@thegardengrant.org