Swahili_Utafiti wa Jamii ya Mkoa wa 1 - Aula ya Matumizi ya Majengo
Katika Mpango makini wa APS wa Mkoa wa 1, uandikishaji wa wanafunzi umekuwa ukipungua kwa miaka. Kupungua kwa uandikishaji huleta changamoto za fedha mambo ambayo tunapaswa kushughulikia ili kutumikia vizuri jamii yetu katika siku zijazo. Hatua muhimu katika kupanga ni kuamua jinsi majengo ya sasa hivi yaliyo katika mkoa yanaweza tumiwa vinginevyo au kutumika kwa njia tofauti kuliko ilivyo sasa. Ili kufanya haya, ni muhimu kwamba tuzingatie maoni kutoka kwa jamii yetu. Zaidi hasa, tungependa kujua ni mahitaji gani ya matumizi ya majengo unayoyaona kama kipaumbele cha kwanza tunapotazamia siku za usoni. Yaani, jinsi gani ungependa kuona majengo ya APS yakitumiwa katika mkoa wako hapo siku za usoni?

Hivi karibuni APS ilipokea maoni kutoka kwa vikundi mahsusi vya jamii vilivyoshirikisha wazazi, walezi, wafanyakazi na wanajamii ambao wanaishi na kufanya kazi katika Mkoa wa 1 wa APS. APS ingependa maoni ya ziada kuhusu mahitaji na shauku za Mkoa wa 1 za matumizi ya majengo katika siku za usoni, ndio sababu tunaomba maoni yenu kupitia utafiti huu. Ni muhimu kufahamu kwamba utafiti huu sio kipengele kikuu kinachoamua jinsi majengo yatatumiwa. Utafiti huu utategemea maoni na ushiriki wa jamii wa awali. Pia kutakuwa na maoni kutoka kwa Kamati ya Ushauri wa Majengo ya Long-Range ambayo inazingatiwa pamoja na uchambuzi wa wafanyakazi. Mwishowe, Bodi ya Elimu ya APS huenda ikahitajika kupigia kura hayo mapendekezo. Tunawashukuru mbeleni kwa kushiriki kwenu na kwa kutoa maoni yenu ya thamani juu ya kazi hii muhimu! Tafadhali kamilisha utafiti ifikapo Ijumaa, Nov.19.

Sign in to Google to save your progress. Learn more
Tafadhali teua chaguo linalokufafanua vizuri: *
Je, umeunganishwa na angalau shule moja katika Mkoa wa 1 (Crawford, Montview, North, Paris, Park Lane, Sable au Altura)?
Clear selection
Miongoni mwa makundi yafuatayo ya matumizi kuu ya majengo, tafadhali chagua ni aina gani ya matumizi ya majengo ambayo ni muhimu sana na/au ya thamani kwako.
Clear selection
Kwa ajili ya matumizi ya elimu au mafundisho, chaguzi zifuatazo zilitambuliwa kuwa na uhitaji wa juu wa jamii kupitia mijadala ya vikundi mahsusi vya Mkoa wa 1. Tafadhali orodhesha chaguzi zifuatazo jinsi jengo linaweza kutumiwa (1 ikiwa kipaumbele cha juu na 3 ikiwa kipaumbele cha chini) kulingana na jinsi unaamini kila chaguzi ni muhimu/ ya thamani.
Shule ya mwelekeo maalum wa mtaala imeunganishwa na mtazamo wa Afya Moja wa Mkoa wa 1. Shule ya mwelekeo maalum wa mtaala iliyopo Mkoa wa 1 inapatikana kwa wanafunzi wote wa APS, bila kujali wanapoishi. Shule hiyo ya mwelekeo maalum wa mtaala itakuwa na masomo yote ya msingi, kama vile hesabu, Kiingereza, sayansi, na somo la jamii, lakini pia litajumuisha mtazamo wa Afya Moja. Afya Moja huchunguza uingiliano kati ya watu, wanyama, mimea na mazingira yao ya pamoja ili kufikiwa matokeo bora ya afya kwa kujifunza taaluma nyingi na kukuza ushirikiano katika sekta zote (k.m. Afya ya binadamu, afya ya mnyama, sayansi ya mazingira, watengeneza sera. nk.)
Programu Mbadala ya Elimu/Upanuzi wa Njia za APS Nafasi ya kupanua na kuhifadhi Njia za APS, programu mbadala ya sekondari ambayo hutoa ratiba ya kujifunza inayobadilika kwa urahisi, kujifunza mtandaoni, masomo ya mseto, na mazingira ndogo ya kusaidia wanafunzi wahitimu.
Chuo cha Mapema cha Sekondari. Chuo cha Mapema cha Sekondari ni aina maalu ya shule ya upili ambayo wanafunzi hupata diploma yao ya shule ya upili na mojawapo ya shahada yao ya mwanzo, sifa zingine za baada ya chuo cha upili, au sifa sitini za kuhitimu chuo katika miaka nne.
1
2
3
Clear selection
Kwa ajili ya huduma za matumizi ya majengo ya mwanafunzi/msaada, chaguzi zifuatazo zilitambuliwa kuwa na uhitaji wa juu wa jamii kupitia mijadala ya vikundi mahsusi vya Mkoa wa 1. Tafadhali orodhesha chaguzi zifuatazo za matumizi ya majengo ndani ya matumizi ya majengo kwa mwanafunzi/huduma za utegemezo (1 ikiwa kipaumbele cha juu na 5 ikiwa kipaumbele cha chini) kulingana na jinsi unaamini kila chaguzi ni muhimu/ya thamani.
Kujifunza kwa vizazi mbalimbali/mafunzo ya watoto na watu wazima. Mahali ambapo panategemeza kujifunza kwa watoto na watu wazima na wakati mwingine kujifunza pamoja.
Nafasi ya fursa za lugha ya Kiingereza/Kihispania. Mahali pa kutegemeza fursa za kujifunza lugha na/au elimu kwa lugha mbili.
Kituo cha Uajiri wa Waalimu, kinachozingatia waalimu wasio weupe. Mahali pa kutegemeza kuajiri na kuendeleza waalimu, hasa waalimu wasio weupe.
Kituo cha Maendeleo ya Watoto/Utunzi wa Watoto Mahali panapotoa utunzi wa watoto au fursa za kujifunza elimu ya watoto wachanga.
Huduma za Wanafunzi wa Kipekee Mahali pa kutegemeza mahitaji maalum ya wanafunzi wenye ulemavu na/au wafanyakazi ambao hutegemeza wanafunzi wenye ulemavu
1
2
3
4
5
Clear selection
Kwa ajili ya matumizi ya jamii, chaguzi zifuatazo zilitambuliwa kuwa na uhitaji wa juu wa jamii kupitia mijadala ya vikundi mahsusi vya Mkoa wa 1. Tafadhali orodhesha chaguzi zifuatazo za matumizi ya majengo ndani ya matumizi ya majengo kwa jamii (1 ikiwa kipaumbele cha juu na 2 ikiwa kipaumbele cha chini) kulingana na jinsi unaamini kila chaguzi ni muhimu/ya thamani.
Kituo cha Msaada/Huduma za Afya ya Akili Mahali ambapo jamii inaweza pata msaada wa afya ya akili na huduma.
Kituo cha Jamii (na au bila huduma za ziada za wraparound). Mahali ambapo jamii inaweza kukusanyika na huduma tofauti kutolewa. Hii pia inaweza kujumuisha mahali pa huduma za ziada ambazo zinaweza kutumikia jamii, kama vile chakula, huduma ya afya, huduma za jamii n.k.
1
2
Clear selection
Ikiwa ungependa, tafadhali shiriki mawazo mengine juu ya aina nyingine za matumizi ambayo ungependa kuona katika Mkoa wa 1.
Submit
Clear form
Never submit passwords through Google Forms.
This form was created inside of APS Google. Report Abuse