Mpendwa,
UNFPA inakushukuru kwa kushiriki katika utafiti huu mfupi.
Utafiti huu ni sehemu muhimu ya Utafiti wa Msingi wa Programu ya UNFPA inayoitwa MASS. Programu ya MASS imeundwa kuziba mapengo
yaliyopo katika programu zinazoshughulikia Ukatili wa Kijinsia unaowezeshwa na
Teknolojia (TF GBV). Progamu hiyo inatekelezwa na Kitengo cha Ufundi cha UNFPA
na Ofisi za Nchi za UNFPA huko Benin na Kenya, kuanzia Februari 2024 hadi Machi
2027. Progamu hiyo itashughulikia TF GBV kwa kutekeleza shughuli katika nguzo
tano: Mwitikio, Kuzuia, Sheria na Sera, Utafiti na Tathmini, na juhudi za
kuunganisha.
Lengo la utafiti huu ni kutoa data ya msingi kwa ajili ya
programu ya MASS. Ujumbe utakaopatikana kupitia utafiti huu mfupi utasaidia
UNFPA kuelewa ufahamu na uzoefu wa watumiaji wa intaneti kuhusu TF GBV ambayo
itatumika kufahamisha upangaji na utekelezaji wa programu ya MASS na itatumika
kufuatilia na kutathmini matokeo ya programu.
Majibu yote ni ya siri na na yatawekwa siri kabisa. Utafiti
unatarajiwa kuchukua takriban dakika 10-15. Mwishoni mwa utafiti, utakuwa pia
na nafasi ya kuongeza maoni mafupi ya ziada ambayo yanaweza kutoa taarifa zaidi
na kutusaidia katika kuimarisha huduma za kuzuia na kukabiliana na TF GBV.
Matokeo ya utafiti yatakuwa sehemu ya ripoti ya Utafiti wa Msingi ambayo
itasambazwa na programu ya UNFPA ya MASS inayohusiana na kuweka mazingira yoye salama.
Tunashukuru sana kwa ushiri wako muhimu. Ukipata swali lolote
tafadhali wasiliana na timu ya utafiti wa msingi kwa: pdewi@unfpa.org.
Kumbuka: Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu
(UNFPA) linafafanua TF GBV kama “kitendo cha unyanyasaji kinachofanywa na mtu
mmoja au zaidi ambacho kinafanywa, kusaidiwa, kuchochewa na kukuzwa kwa sehemu
au kikamilifu kwa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ya habari au vyombo vya
habari vya digital, dhidi ya mtu kwa misingi ya jinsia zao.